Heshima kwenu wadau,
Kibiashara kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara hasa kwa zile zinazoanza ingawa nyingi kati ya hizo ni NGUMU sana, hivyo kupelekea watu wengi kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini hushindwa kuyafanikisha kutokana na mitaji. Kwa mtazamo wangu, naona kama ukitumia njia ya kuomba fedha kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi walio karibu yako, wanaokuamini, kukuheshimu, kukufahamu na wenye uwezo kiasi itakuwa njia rahisi ukilinganisha na mikopo kutoka taasisi za kifedha ambapo utajikuta unafanya biashara kwa presha na hofu ya kurejesha deni. unaweza kufanya kama ifuatavyo kwa kuchukulia uhitaji wa mtaji wa Tsh 10,000,000:

1 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 100,000 kutoka kwa watu 100 = Tsh 10,000,000
2 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 200,000 kutoka kwa watu 50 = Tsh 10,000,000
3 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 350,000 kutoka kwa watu 30 = Tsh 10,000,000
4 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 500,000 kutoka kwa watu 20 = Tsh 10,000,000
5 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 1,000,000 kutoka kwa watu 10 = Tsh 10,000,000

NB: - Naamini tunafahamiana na watu wengi sana tangu mtoto unakua hadi hapo ulipo, kuanzia uliocheza nao, marafiki wa primary, sekondary, vyuo, kazini, majirani, ndugu, jamaa, marafiki, marafiki uliojuana nao kwenye mitandao kama JF, Facebook, Twitter nk..nina hakika hutakosa watu wasiopungua 100 wenye nia, uelewa na uwezo wa kukufanikishia hili.
- Uhitaji, madhumuni ya kuomba, muda wa kurejesha, malengo ya matumizi inategemea na makubaliano yako na unayemuomba, na si lazima hao watu utakao waomba wajue kusudio lako la njia hii ya kupata mtaji, pia usiombe kama msaada, omba kama mkopo ili baada ya muda mfupi kama miezi miwili ama mitatu uahidi kurejesha.
- Nina imani kiasi cha Tsh 10,000,000 ni mtaji tosha kwa biashara ndogo ndogo kwa kuanzia. Mfano: jiko la baa, kibanda cha chips, salon ya kiume, stationary, internet cafe, duka la jumla, duka la kawaida, genge, grecery, bajaji, duka la nguo hasa mitumba bomba nk.. ambapo itakuwa rahisi kwako kwa muda wa miezi mitatu kuweza kurejesha fedha ulizoomba.