Njia rahisi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara
Heshima kwenu wadau,
Kibiashara kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara hasa kwa
zile zinazoanza ingawa nyingi kati ya hizo ni NGUMU sana, hivyo
kupelekea watu wengi kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini
hushindwa kuyafanikisha kutokana na mitaji. Kwa mtazamo wangu, naona
kama ukitumia njia ya kuomba fedha kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi
walio karibu yako, wanaokuamini, kukuheshimu, kukufahamu na wenye uwezo
kiasi itakuwa njia rahisi ukilinganisha na mikopo kutoka taasisi za
kifedha ambapo utajikuta unafanya biashara kwa presha na hofu ya
kurejesha deni. unaweza kufanya kama ifuatavyo kwa kuchukulia uhitaji wa
mtaji wa Tsh 10,000,000:
1 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 100,000 kutoka kwa watu 100 = Tsh 10,000,000
2 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 200,000 kutoka kwa watu 50 = Tsh 10,000,000
3 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 350,000 kutoka kwa watu 30 = Tsh 10,000,000
4 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 500,000 kutoka kwa watu 20 = Tsh 10,000,000
5 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 1,000,000 kutoka kwa watu 10 = Tsh 10,000,000
NB: - Naamini tunafahamiana na watu wengi sana tangu mtoto unakua hadi
hapo ulipo, kuanzia uliocheza nao, marafiki wa primary, sekondary, vyuo,
kazini, majirani, ndugu, jamaa, marafiki, marafiki uliojuana nao kwenye
mitandao kama JF, Facebook, Twitter nk..nina hakika hutakosa watu
wasiopungua 100 wenye nia, uelewa na uwezo wa kukufanikishia hili.
- Uhitaji, madhumuni ya kuomba, muda wa kurejesha, malengo ya
matumizi inategemea na makubaliano yako na unayemuomba, na si lazima hao
watu utakao waomba wajue kusudio lako la njia hii ya kupata mtaji, pia
usiombe kama msaada, omba kama mkopo ili baada ya muda mfupi kama miezi
miwili ama mitatu uahidi kurejesha.
- Nina imani kiasi cha Tsh 10,000,000 ni mtaji tosha kwa biashara
ndogo ndogo kwa kuanzia. Mfano: jiko la baa, kibanda cha chips, salon ya
kiume, stationary, internet cafe, duka la jumla, duka la kawaida,
genge, grecery, bajaji, duka la nguo hasa mitumba bomba nk.. ambapo
itakuwa rahisi kwako kwa muda wa miezi mitatu kuweza kurejesha fedha
ulizoomba.
No comments:
Post a Comment