Je, wajua njia/mbinu za kutangaza biashara yako?
Waswahili wanasema, kizuri kula na mwenzio.
Natumai
maarifa haya yatawafaa wengi wenu ambao mnafikiria kuanzisha biashara au
mlio na biashara pia, mnahitaji kujua njia/ mbinu za kutangaza
biashara zenu.
1.Jitambulishe/Watambulishe
wengine- Wenzetu katika lugha ya Kiingereza wanaita kitu hiki
“networking”. Kwa bahati mbaya, Kiswahili hakina neno mbadala la moja kwa moja
kuhusu “networking” hii. Kwa kifupi, ni kwamba ukiwa na biashara, kila
unayekutana naye anaweza kuwa mteja wako.Jitambulishe bila aibu.Mjue na yeye
akujue, mwambie unachokifanya(biashara yako).Pia usisahau marafiki zako.Je
marafiki zako wanajua unachokifanya? Watu wengi huwa wanasahau kwamba marafiki
wanaweza kuwa chanzo kizuri sana cha mauzo au kuongezeka kwa idadi ya
wateja.Waambie marafiki zako na wao(hususani kama ni marafiki kweli) bila shaka
watawaambia marafiki zao pia.
1.Kuwa
na tovuti (website)- Katika zama za leo,ni muhimu kwa biashara kuwa na
tovuti. Natambua kwamba sio biashara zote zinaweza au zina uwezo wa kuwa na
tovuti. Unachotakiwa hapa ni wewe mwenyewe kujiuliza, je aina hii ya biashara
niliyonayo inahitaji uwepo wa mtandaoni kupitia tovuti? Ni swali na jibu ambalo
wewe mwenyewe sharti ulipatie majibu. Uzuri wa tovuti au uwepo wa mtandaoni ni
kwamba hata pale biashara yako inapokuwa imefungwa(usiku kwa mfano kwa biashara
za mchana) bado unakuwa unaendelea kuitangaza.
1.Mitandao
Jamii Ni Lazima- Sidhani kama natakiwa kusisitiza zaidi jinsi gani ni
muhimu kutangaza huduma au bidhaa zako kupitia mitandao jamii kama vile Blogs,
Facebook,Twitter,LinkedIn,Google Plus etc. Kama unapenda kuandika,kwa mfano,
anzisha blog.Andika,weka video za huduma unazozitoa.Siku hizi kamera nyingi
zina uwezo wa kuchukua video.Kwanini usijichukue video ya dakika mbili
ukielezea bidhaa au huduma unazozitoa na kutuma mtandaoni kupitia mitandao
jamii? Bila shaka marafiki zako watakupata vizuri zaidi na wao wanawapelekea
wengine video hiyo.Ujumbe utaenea.
1.Orodhesha
Biashara Yako katika Huduma Za Orodha Za Biashara-
Hatua muhimu katika biashara ni kutambulika. Njia mojawapo nzuri ya kuchukua au
kufikia hatua hii ni pamoja na kujiorodhesha. Kwa mfano,biashara yako
inahusiana na mazao ya kilimo.Kama kuna umoja/ushirikiano wa wafanyabiashara wa
mazao ya kilimo hakikisha kwamba jina lako na la biashara yako yanakuwepo
katika orodha hiyo. Pia katika nchi mbalimbali zipo huduma za kujiorodhesha
zinazoitwa Kurasa Za Njano(Yellow Pages). Hakikisha kwamba biashara yako ipo
ndani. Pia search engines kama vile Google,Yelp,Yahoo,Bing nk zinazo huduma
mbalimbali za kuorodhesha biashara mbalimbali katika nchi. Itumie fursa hiyo.
Angalizo: Katika kujiorodhesha kuwa makini,zipo huduma za Bure na Za
Kulipia.Kazi Ni Kwako.
1.Tumia
Barua Pepe Kutangaza/Kujitangaza-Siku hizi watu wengi wana
e-mail address(anuani pepe). Bila shaka hata wewe msomaji unayo.Kwanini basi
usiitumie hiyo anuani pepe kuwasiliana na wateja wako?Anapokuja kwenye sehemu
yako ya biashara,muombe mteja anuani pepe yake ili panapokuwa na “deal”
umtumie.Mara nyingi hakuna atakayekataa. Kila mtu anapenda “deal”.Ukishakuwa na
anuani pepe,kwanini usimkumbuke mteja wako aidha kwa “deal” au kumtumia e-card
ya X-mas,Eid nk? Angalizo: Usiwatumie wateja wako mambo mengi mengi mara
kwa mara.Wanaweza dhani ni spammers na hivyo waka-block kabisa barua
pepe kutoka kwako.
1.Gawa
Business Cards- Niliwahi kusikia kisa cha jamaa fulani ambaye
alitengeneza business cards nzuri sana. Alipoona ni nzuri sana akagoma
kuzigawa.Akawa anaenda nazo kwenye mikutano nk lakini hazigawi.Unajua
kilichotokea? Biashara ikafa akabaki na business cards zake.Nnachotaka kusema
ni kwamba kila fursa inapojitokeza,gawa business cards zako.Na usigawe tu na
kutosema kitu.Mwambie kwa maneno machache yule unayempatia business card kuhusu
biashara yako. Muombe na yeye akupe business card yake kama anayo. Kwa maneno
mengine ukifanya hili unakuwa pia umefanya lile nililolizungumzia mwanzoni
kabisa.
1.Shiriki
Katika Huduma/Shughuli za Kijamii- Kama mfanyabiashara,njia
mojawapo rahisi ya kuifanya jamii ikutambue ni pamoja na kushiriki katika
shughuli mbalimbali zinazoendelea katika jamii. Unaweza kushiriki kama mdhamini
au mfanyakazi wa kujitolea. Mara nyingi huduma/shughuli hizi za kijamii huwa
zinahudhuriwa na watu wa habari(media) na kwa maana hiyo unaweza kuwa umepata
“matangazo bila kulipia”. Lakini cha muhimu zaidi ni kwamba unaposhiriki katika
shughuli za kijamii ni ishara kwamba unaijali jamii hiyo. Unapofanya hivyo ni
rahisi na wewe kuungwa mkono na wana jamii hao.
1.Muombe
Mtu(mwandishi,blogger,mtangazaji nk) afanyie mapitio(review) bidhaa yako-
Utaratibu huu bado haujaingia sana nchini kwetu.Lakini mimi binafsi naukubali
sana. Kama unauza bidhaa fulani na unaamini kwamba bidhaa yako ni
bora,utafaidika sana endapo mtu kama mwandishi,blogger,mtangazaji wa
televisheni,radio nk,atakapoitumia bidhaa yako,kuona matokeo yake na kisha
kwenda hewani na kuwaambia wanaomsikiliza kuhusu bidhaa aliyoitumia. Naomba
nisisitize hapa kwamba ni muhimu akawa ameitumia kweli na kupata matokeo
anayoyapigia debe.Kinyume chake ni kwamba yeye ataharibu heshima yake na wewe
utakuwa umekosa lundo kubwa zaidi la wateja. Angalizo: Kuna waandishi au
bloggers na watangazaji nk ambao hawafanyi mapitio BURE..Ongea nao muelewane.
1.Hudhuria
na Tumia Vizuri Maonyesho Ya Biashara/Mikutano-Sio
kila biashara inaweza kushiriki katika maonyesho ya biashara hususani yale
makubwa kama vile Saba Saba au Nane Nane.Lakini yapo maonyesho mengine
mbalimbali(mfano kupitia wizara za serikali au umoja fulani wa
wafanyabiashara). Kila inapowezekana,usilaze damu.Shiriki.Pia shiriki mikutano mbalimbali
inayoandaliwa kwa ajili ya wafanyabiashara fulani. Kwa uzoefu wangu,mikutano ya
aina hii ipo na inafanyika mara kadhaa tena bila malipo.Shiriki.Unapokwenda
huko beba kadi zako za biashara,vipeperushi nk.Gawa,ongea na wenzako,toa
mchango na mawazo yako.
1.Tangaza
Kwenye Magazeti,Televisheni,Radio,Blogs Nk: -Miongoni mwa
njia/mbinu zote nilizozitaja hapo juu,pengine hii ndio ikawa ya gharama zaidi.
Lakini ukweli ni kwamba matangazo,yanalipa kwa maana ya kwamba,kama uwezo
upo,basi angalia uwezekano wa kutangaza kupitia njia hizi. Lakini kitu kimoja
ambacho ni vizuri kukizingatia hapa ni kwamba unapoamua kutangaza kupitia njia
hizi,kuwa mbunifu.Usifanye tu kile ambacho washindani wako wa kibiashara
wanafanya. Jaribu kuwa na mawazo huru na binafsi. Pasua kichwa,fikiri.
No comments:
Post a Comment